1 Mei 2022 - 18:52
Waafghani waandamana mjini Rome kulaani mauaji ya kigaidi Misikitini Afghanistan

Raia kadhaa wa Afghanistan wanaoishi nchini Italia wamekusanyika mjini Rome kulaani wimbi la mashambulio ya kigaidi lililoyakumba maeneo tofauti ya Afghanistan.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kwa mujibu wa shirika la habari la Iran Press waandamanaji hao walikuwa wanapiga nara za kulaani mauaji ya kigaidi na ya kinyama yanayofanywa katika shule na Misikiti huko Afghanistan ikiwemo inayosema: "Komesheni mauaji ya kimbari dhidi ya Wahazari."

Kabul, mji mkuu wa Afghanistan na maeneo mengine mbalimbali ya nchi hiyo, imekumbwa na mashambulizi mengi ndani ya mwezi huu wa mtukufu wa Ramadhani. 

Shambulio lililotokea kwenye shule ya Abdul Rahim Shahid huko magharibi mwa Kabul liliua shahidi wanafunzi wasiopungua 27 na kujeruhi wengine zaidi ya 100 hivi karibuni.

Waafghani wenye hasira wamekusanyika mbele ya ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Rome Italia kulaani jinai hizo na kutaka kulindwa roho za raia wakiwemo Waislamu wa kabila la Hazara huko Afghanistan. 

342/